Business

header ads

MKUU WA USALAMA RWANDA AKAMATWA

Mkuu wa Usalama wa Rwanda Karenzi Karake, ambaye alikuwa anatafutwa nchini Hispania kwa makosa ya uhalifu wa kivita amekamatwa Jijini London.

Polisi wa nchi hiyo wa kitengo cha kubadilishana uhalifu wamemkamata Jenerali Karake, katika uwanja wa ndege wa Heathrow siku ya jumamosi, imefahamika hii leo.

Jenerali Karake mwenye umri wa miaka 54, atabakia kizuizini hadi siku ya Alhamis, baada ya kufikishwa kwenye mahakama ya Westminster.

Jenerali Karake anatuhumiwa kuagiza mauaji wakati akiwa Mkuu wa Intelejensia katika jeshi wakati wa machafuko ya mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 nchini Rwanda.

Post a Comment

0 Comments