Business

header ads

KELELE NYINGI ZA MAGARI HUPUNGUZA UMRI WA MTU KUISHI.


Utafiti wa madaktari umebaini kuwa kuishi katika eneo lililojirani na kelele za magari kunaweza kumpunguzia muda wa mtu kuishi na kuongeza hatari ya kupata ugonjwa wa kiharusi.

Watafiti wamelinganisha kiwango cha kelele na takwimu za vifo na wagonjwa waliolazwa Jijini London, na kuelezea katika chapisho lao la Jarida la Moyo la Ulaya.

Katika maeneo ambayo wakati wa mchana kelele za magari barabarani zinazidi kipimo cha kelele cha dezibeli 60, yalikuwa na vifo asilimia nne zaidi kuliko maeneo yasiyo na kelele ambayo kelele zilikuwa dezibeli 55 ama chini ya hapo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeweka kiwango cha kelele cha dezibeli 55 ni cha mwisho kuwapo kwa jamii, ambapo juu ya hapo husababisha matatizo ya kiafya.

Post a Comment

0 Comments