Business

header ads

CNDD FDD CHASUSIA MAZUNGUMZO

Chama tawala nchini Burundi CNDD FDD kimesema kinasusia mazungumzo yanayosimamiwa na Umoja wa Mataifa ya kuutafutia ufumbuzi mzozo wa kisiasa nchini humo kati yake na vyama vya upinzani.

Mazungumzo hayo yaliyofanyika hii leo yamehudhuriwa na wanasiasa wa vyama vya upinzani ,wawakilishi wa asasi za kiraia na viongozi wa kidini lakini chama tawala CNDD FDD pamoja na ofisi ya rais hawakutuma mwakilishi.

Kiongozi wa chama hicho tawala Pascal Nyabenda amesema chama hicho kinalijulisha taifa na jumuiya ya kimataifa kuwa jambo wanalolipa kipaumbele hivi sasa ni kuendelea kwa kampeini za chaguzi na hivyo haitashiriki katika mazungumzo katika kipindi hicho cha kampeni na kuyataja mazungumzo hayo kuwa yanalenga kutatiza chagauzi zijazo.

Post a Comment

0 Comments