Business

header ads

BUNGE LAPITISHA BAJETI YA SHILINGI TRILIONI 22.4

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limepitisha Bajeti ya Serikali ya shilingi trilion 22.4 kwa mwaka wa fedha 2015/2016 iliyowasilishwa june 11 mwaka huu na Waziri wa Fedha na uchumi Mh. Saada Mkuya Salum ambayo imefanyiwa marekebisho kadhaa.

Akijibu hoja za Wabunge kuhusu bajeti hiyo Waziri Mkuya amesema kuwa moja ya maeneo yaliyofanyiwa marekebisho ni Pensheni ya Wazee wastaafu Utumishi wa Umma kwa kupandisha hadi shilingi laki moja kutoka elfu 85 iliyopandishwa kutoka sh. elfu 50 ya awali.

Waziri Mkuya ameongeza kuwa kutokana na ufisadi uliyopelekea kupotea zaidi ya shilingi bilioni 6 za wazee wote, serikali imeandaa mfumo maalumu wa kuwatambua

Aidha Mh. Mkuya amewataka wananchi waendelea kuchangia maendeleo ya nchi kutokana na tozo ya mafuta ambayo iliongezwa kwa ajili ya kuchangia sekta ya Umeme Vijijini pamoja na Mfuko wa Maji.

Post a Comment

0 Comments