Business

header ads

ZITTO KABWE AMESEMA HAJAPATA TAARIFA RASMI KUTOKA KWA SPIKA WA BUNGEMbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe amesema hajapata taarifa rasmi kutoka kwa Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda, ikimtaarifu kuvuliwa uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), hatua inayomwondolea sifa za kuwa mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Kigoma Kaskazini.

Akizungumza na East Africa Radio muda mfupi baada ya kuendesha vikao vya kamati ya bunge ya hesabu za serikali akiwa kama Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Kabwe amesema hivi sasa anaendelea na kazi kama kawaida na kwamba ataachia ngazi wadhifa wa ubunge punde atakapopata taarifa rasmi ya maandishi kutoka ofisi ya Spika Anne Makinda.

Kauli hiyo ya Mh. Kabwe inafuatia maamuzi ya kumvua uanachama wa Chadema, maamuzi yaliyofikiwa baada ya chama chake hicho kushinda kesi katika shauri ambalo mbunge huyo alilifungua katika mahakama kuu ya Tanzania, akikitaka chama chake kisimjadili kutokana na tofauti zilizokwepo baina ya pande hizo mbili.

Post a Comment

0 Comments