Business

header ads

WATOTO NJITI 9000 HUFA KILA MWAKA NCHINI TANZANIA KATI YA WATOTO LAKI MBILIWatoto 9,000 wanaozaliwa kabla ya kufikisha miezi tisa hufariki dunia kati ya watoto laki mbili na elfu kumi na tatu wanaozaliwa kila mwaka nchini Tanzania .

Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dar es Salaam wakati Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mahmoud Thabit Kombo akizindua mkakati wa taasisi ya Doris Molel wa kukabiliana na vifo vya watoto hao ambao hujulikana kama njiti.

Mh. Kombo amesema kuwa ni jukumu la Watanzania wote kuhakikisha wanawalinda wanawake wajawazito kisaikolojia sambamba na kuzingatia lishe kwa wanawake hao ili kuondokana na matatizo ya wanawake kuzaa watoto njiti

Post a Comment

0 Comments