Business

header ads

WATANZANIA 443 WANASHIKILIWA KATIKA NCHI KADHAA KWA KUJIHUSISHA NA DAWA ZA KULEVYA

Tanzania imefanikiwa kudhibiti zaidi ya tani 2.3 za dawa za kulevya zilizokamatwa na vikosi vya wanamaji huku za zaidi ya watanzania 443 wamekamatwa katika nchi mbalimbali duniani wakihusishwa na usafirishaji na utumiaji wa dawa za kulevya.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa ripoti ya dawa za kulevya ya Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Kudhibiti Dawa za Kulevya na Makosa ya Jinai (UNODC) Mwakilishi kutoka Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Tanzania Bw. January Ngisi amesema tatizo la dawa za kulevya katika ukanda wa Afrika Mashariki bado ni kubwa na kueleza kwa kushirikiana na vyombo vya dola wameridhia mikataba ya kupunguza upatikanaji wa dawa za kulevya.

kwa upande wake Afisa Uhusiano wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bi. Stela Vuzo amesema ripoti hiyo imeitaka serikali kuwasaidia watoto wasijingize katika matumzi ya dawa za kulevya ambazo zimekuwa na madhara makubwa ikiwemo athari za kiafya na iwekwe mikakati itakayotokomeza uingizwaji na utumiaji wa dawa za kulevya nchini .

Post a Comment

0 Comments