Business

header ads

WAKAZI WA BUGURUNI WAYAHAMA MAKAZI YAO, WATIMULIWA NA MVUA ZA DAR ES SALAAM


 Wakazi wa Buguruni kwa Mnyamani, jijini Dar es Salaam, wakihamisha vitu ndani ya nyumba zao na mifugo ili kukimbia mafuriko yaliyotokana na mvua kumbwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam, kuanzia juzi. Maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam, yamekumbwa na mafuriko hayo siku ya leo baada ya mvua kubwa iliyonyesha hii leo, ambapo imeelezwa kuwa mvua hizi bado zitaendelea kunyesha.
 ''Tunahama kwa muda tu mvua ikiisha tutarejea kwenye nyumba zetu'', hii ndiyo imekuwa ni kawaida kabisa kwa wakazi wa jijini Dar es Salaama, na hasa kwa wale wanaoishi maeneo yanayojaa maja ambao wamekuwa wakisisitizwa kuhama kabla ya kukumbwa na kadhia kama hii na wao kuwa wakaidi hadi yanapowakuta mafuriko kama haya.
''Tunasogea kwenye vituo vya mabasi yaendayo kasi kujishikiza'', Wananchi wengi waliokumbwa na kadhi hii wamekuwa wakikimbilia kwenye Vituo vya mabasi yaendayo kasi na kuweka makazi kwa muda ambapo ukipita maeneo ya Jangwani utawakuta wengi tu.


Post a Comment

0 Comments