Watu
42 wamefariki dunia na wengine 23 kujeruhiwa baada ya basi
walilokuwa wakisafiria kutoka Mbeya kuelekea Jijini Dar es Salaam
kugongana na Lori la mizigo na kisha kuangukiwa na kontena katika mji
mdogo wa Mafinga wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Akizungumzia
ajali hiyo Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi
amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa tano asubuhi ikihusisha
basi la kampuni ya Majinja lenye namba za usajili T 438 CDE na lori
lenye nambari za usajili T 689 APJ.
Kamanda
Mungi amesema chanzo cha ajali hiyo ni madereva wa magari yote
mawili kujaribu kukwepa shimo kubwa lililopo barabarani na ndipo
kontena lililobebwa katika lori kuchomoka na kuligonga gari na watu
22 kufariki dunia papo hapo na 20 wamefariki dunia wakati wakipelekwa
hospitali kwa ajili ya matibabu
Mungu azipokee na kuzilaza mahala pema peponi roho za marehemu wote katika ajali hii na awajaalie kupona kwa haraka majeruhi wote.
0 Comments