Business

header ads

RAIS MKAPA ATAKA ELIMU YA UWEKEZAJI KUTOLEWA KWA WANANCHIRais mstaafu wa awamu ya tatu nchini Tanzania Mh. Benjamini Mkapa ametaka kutolewa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu uwekezaji kutokana na imani waliyonayo wananchi kwamba mtu anyetaka kuja kuwekeza anafanya hivyo kwa maslahi yake binafsi.

Mhe. Mkapa amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati taasisi inayoshughulikia mazingira ya uwekzaji barani Afrika ICF na kituo cha uwekzaji nchini TIC walipokuwa wakitiliana saini makubaliano ya kusaidia kuvutia na kuongeza uwekezaji wa ndani na nje hapa nchini.

Amesema bado kuna tatizo la uelewa kuhusu uwekezajina masuala ya kisiasa nayo yamekuwa yakichangia hivyo ameshauri kutumika ipasavyo kwa kituo cha uwekezaji nchini TIC katika masuala yote ya uwekezaji ili kuleta usawa kati ya wawekezaji wa ndani na wale wa nje wanaokuja kuwekeza Tanzania.

Post a Comment

0 Comments