Business

header ads

RAIS KIKWETE ATAKA UWEKEZAJI UKANDA YA KATI UBORESHE USTAWI WA MAISHA YA WANANCHI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania amesema kuna haja ya kuhakikisha kuwa uendelezaji wa na uwekezaji katika ukanda wa kati wa miundombinumaendeleo, unalengapiatika kuboresha stawi wa maisha ya raia wa nchi hizo.

Aidha, rais Kikwete ameaema Tanzania inakusudia kupunguza vizuizi vya barabarani katika barabara kuu kati ya Dsm na nchi jirani za Uganda, Rwanda na Burundi, kutoka vizuizi zaidi ya kumi hadi vizuizi vitatu.

Akizungumza katika siku ya kwanza ya mkutano wa wakuu wa nchi zinazounda ukanda wa kati wa maendeleo, rais Kikwete amesema mipango hiyo iangalie pia namna ya kuboresha mawasiliano na upatikanaji wa nishati ya uhakika, ambapo ameshauri umuhimu wa ushirikiano ambapo nchi yenye hazina kubwa ya nishati inaweza kusambaza na kuuza kwa nchi jirani, na hivyo hivyo kwa suala la mawasiliano.

Kwa upande wake, rais wa Uganda Yoweri Museveni amewataka wananchi wa nchi zinazounda ukanda wa kati wa maendeleo kufanya kazi kwa bidii huku wakitambua vikwazo vinavyozuia ustawi wa jamii ambavyo ni rushwa, ukosefu wa usalama, ukosefu wa masoko na ukosefu wa miundombinu bora.

Mkutano huo wa siku mbili, unakutanisha wakuu wa nchi zote wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ukiwa na lengo la kuchochea maendeleo katika ukanda wa kati kupitia uboreshaji wa miundombinu ya usafirishaji mizigo na bidhaa, mkutano ambao pia umewakutanisha wadau wa sekta ya usafiri, taasisi za kikanda pamoja na vyombo vya kifedha ambavyo ni wafadhili wakuu wa miradi ya miundombinu.


Hata hivyo, viongozi muhimu watatu hawakuhudhuria mkutano wa leo, akiwemo rais Paul Kagame wa Rwanda, rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na rais Laurent kabila kutoka DRC.

Post a Comment

0 Comments