Business

header ads

MVUA YAUWA WATU 39 NA KUJERUHI WENGINE 69 WILAYANI KAHAMA, MKOANI SHINYANGA.

Zaidi ya watu 39 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 69 wamejeruhiwa baada ya nyumba zao kuwaangukia na kuwafunika usiku wa kuamkia leo kufuatia mvua kubwa iliyonyesha wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.

Taarifa zilizothibitishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya amesema mvua hiyo kubwa iliambatana na upepo mkali, hivyo nyumba nyingi zilianguka na nyingine kuezuliwa na kuharibiwa kabisa.

Bw. Mpesya amesema hadi majira ya asubuhi walikuwa wamefanikiwa kupata miili ya watu 39 waliopoteza maisha baada ya kufukua nyumba nyingi, na majeruhi wamekimbizwa hospitali ya wilaya kwa matibabu zaidi.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema nyumba nyingi zimeanguka na zoezi la kutafuta watu waliojeruhiwa au kupoteza maisha bado linaendelea kwa kasi.

Post a Comment

0 Comments