Business

header ads

MGOMO WA WAFANYABIASHARA WATIKISA MKOANI KILIMANJARO
Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa nje ya maduka yao mara baada ya kuamua kuyafunga kwa kile wanaochodai kufanya mgomo kwa lengo la kumuunga mkono Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Johnson Minja ambaye kesi yake inasikilizwa mkoani Dodoma.


Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa baadhi ya maduka yaliyoko Double road.


Maduka yaliyopo katika jengo la Halmashauri ya manispaa ya Moshi lenye ghorofa mbili pia hali ilikuwa hivi.


Pilika pilika zilizozoeleka katika kituo kikuu cha mabasi mjini Moshi hazikuonekana katika kituo hicho,kufuatia mgomo wa wafanyabiashara wa maduka kutofungua kwa kile kinachodaiwa kuungana kwa wafanyabiashara hao katika mgomo.

Wafanyabiasha wa maduka makubwa mkoani Kilimanjaro wamefunga maduka kwa muda usiojulikana kwa madai ya  kugomea   mashine za kieletroniki (EFD) pamoja na kulalamikia mamlaka ya mapato nchini TRA kuongeza kodi kwa asilimia mia moja.
Wafanyabishara hao wamesema wamelazimika kufunga maduka yao kutokana na kulalamikia mamlaka ya mapato nchini kupandisha kodi kwa asilimia mia moja bila kuwashirikisha, sanjari na kushindwa kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki.
Katibu wa chama cha wafanyabiashara mkoa wa Kilimanjaro Bw. Mmasi Sambuo amesema mpaka sasa wafanyabiashara hawajalipa kodi na kwamba kama serikali haitasikiliza malalamiko ya wafanybishara hao watajiondoa kwenye biashara ikifika Aprili Mosi mwaka huu.
Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato nchini tra mkoa wa Kilimanjaro Bw. Abdul Mapembe amesema anasikitishwa na hatua ya wafanyabiashara kufunga maduka kwa kuwa viongozi wa chama hicho walitakiwa kuwasilisha changamoto zinazowakabili wafanyabiashara ili zitafutiwe ufumbuzi kwa mkoa na taifa kwa ujumla.
Wakati huo huo Mahakama mkoani Dodoma imefuta dhamana ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja kutokana na kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa ikiwemo ya kutowazuia wafanyabiashara kufunga maduka yao wakati kesi yake ikiendelea mahakamani.
Akitoa taarifa mbele ya hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Dodoma, Rebecca Mbilu, Mwendesha mashtaka wa serikali Rose Shio amesema kuwa upelelezi dhidi ya kesi hiyo umeshakamilika na kuiomba mahakama kutengua dhamana ya mshtakiwa kutokana na kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa.
 Amesema kuwa pamoja na hilo Mwenyekiti huyo amekuwa akiendelea kufanya mikutano na wafanyabiashara kwa ajili ya kuwahamasisha wasiendelee kulipa kodi kwa kutumia mashine za kielektroniki za efds kitenda alichosema kuwa ni kukiuka masharti ya dhamana aliyopewa.
wakili wa mshtakiwa, Godfrey Wasonga amesema mwenyekiti huyo hakuwashawishi wafanyabiashara nchini kufunga maduka yao bali ni wafanyabishara wenyewe ndo walioamua kufunga maduka yao kwa ajili ya kwenda kusikiliza kesi ya mwenyekiti wao.
Hata hivyo hakimu Mbilu amesema kuwa ameridhika na hoja za upande wa mashtaka na hivyo akatengua dhamana ya Minja na kumtaka kubaki rumande hadi April Mosi mwaka huu ambapo kesi yake itatajwa tena.
Amesema kuwa kesi hiyo itaanza kusikilizwa kwa maelezo ya awali April 9 mwaka huu kutokana na ushahidi wa kesi hiyo kukamilika.Post a Comment

0 Comments