Business

header ads

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAELIMISHA UMMA KUHUSU MAWINGU YENYE KULETA MAAFA

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini Tanzania (LHRC), kimesema kuwa hukumu ya kifo haiwezi kuwa suluhisho la kumaliza vitendo vya ukatili na mauaji yanayofanywa dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi albino.

Mkurugenzi wa Kituo hicho Dkt. Hellen Kijo-Bisimba amesema hayo leo wakati akitoa maoni na msimamo wa kituo chake kuhusu hukumu ya kifo iliyotolewa wiki iliyopita kwa watuhumiwa wa mauaji ya albino, huku matukio ya mauaji na ukatili dhidi ya albino yakiwa bado yanaendelea.

Dkt. Bisimba amefafanua kuwa utafiti uliofanywa kuhusu hukumu hiyo hauonyeshi kuwa imefanikiwa kumaliza matukio ya mauaji na kwamba kuna haja ya nchi kukaa na kufikiria mbinu pamoja na mkakati wa kumaliza matukio hayo na sio kuelekeza nguvu kubwa kwenye suluhisho la kisheria.

Post a Comment

0 Comments