Business

header ads

MAMLAKA YA HALI YA HEWA YAELIMISHA UMMA KUHUSU MAWINGU YENYE KULETA MAAFAMamlaka ya Hali ya Hewa nchini Tanzania TMA imeuelimisha umma wa watanzania juu ya namna ya kutambua wingu linalosababisha mawimbi makali, radi na mvua yenye athari ijulikanayo kwa lugha ya kitaalam TONARDO.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa TMA Dkt. Agnes kijazi amesema kuwa Tonardo inaweza kuwa na athari endapo itatokea kwenye maeneo yanayoishi watu, hivyo ni vyema watanzania wakafuatilia taarifa za TMA kwa karibu ili kufahamu dalili zake.

Dkt. Kijazi ameongeza kuwa Tonardo hutokea mara chache katika mataifa mbali mbali ya afrika, lakini ni vyema dalili zake zikatambulika mapema, ili wananchi waweze kuchukua tahadhari iwapo itatokea hapa nchini

Post a Comment

0 Comments