Business

header ads

DKT. BILAL TANZANIA YAWEZA KUW ANA MAJENGO YENYE KUZINGATIA MAZINGIRA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano mkuu wa kwanza wa Washirika Majenzi ya Kijani wa Afrika Mashariki, uliofanyika leo Machi 19, 2015 kwenye Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Tuzo, Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, PSPF, Adam Mayingu, wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kwanza wa Washirika Majenzi ya Kijani wa Afrika Mashariki, uliofanyika leo Machi 19, 2015 kwenye Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

MAKAMU wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, amesema Tanzania inaweza kuwa na miji yenye maendeleo endelevu iwapo taasisi zinazowekeza
katika ujenzi wa maghorofa na nyumba zenye gharama nafuu zitazingatia uhifadhi wa mazingira ili kuwapunguzia wananchi gharama za maisha.

Akifungua mkutano wa Baraza la Ujenzi Endelevu na Mazingira la Afrika Mashariki (EAGBC) jijini hapa leo, Dk Bilal, amesema ujenzi huo
utafanya miji na wakazi wake kutumia umeme na maji kidogo na pia kusindika majitaka kwa matumizi mengine na kupanda miti ambayo itakuwa
ikinyonya hewa ukaa.

Amesema hali hiyo itawasaidia wakazi kupunguza gharama za maisha kwa sababu nyumba hizo zitajengwa kwa kuzingatia matumizi kidogo ya umeme,
maji na kusindika majitaka yaweze kutumika kwa matumizi mengine ya kibinadamu.

Dk. Bilal amesema kwa mfano, licha ya miji katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuwa katika hatua mbalimbali za maendeleo,
lakini nchi zote hizo tano zipo katika kundi la nchi zinazoendelea.

Amesema utekelezaji, uendelezaji na uwezeshaji wa kifedha katika ujenzi unaozingatia mazingira, unatakiwa uanze kwenye sera, kubuni na
teknolojia ambayo itahifadhi maajabu asilia na kuhidhi uendelevu wa jumuiya.

Mkutano huo wa siku mbili uliowajumuisha washiriki zaidi ya 200 ambao ni wadau mbalimbali wa ujenzi kutoka Singapore, EAC, Shirika la Nyumba
la Taifa (NHC) na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) zilikuwa ni miongoni mwa taasisi ambazo zilitunukiwa cheti kwa ujenzi wa nyumba
zao unaozingatia hifahi ya mazingira.

Pia Mkamu wa Rais ametunukiwa cheti kwa kuwa mstari wa mbele katika kuhifadhi mazingira nchini.

Akizungumza baada ya ufunguzi wa mkutano huo, Rais wa Baraza la Ujenzi Endelevu na Mazingira, Mhandisi Ngwisa Mpembe, alisema Tanzania
imepiga hatua kubwa katika miaka ya hivi karibu kwa taasisi wadau wa ujenzi kujenga nyumba zinazozingatia hifadhi ya mazingira, licha ya
jiji la Dar es Salaam kuwa na masterplan ya muda mrefu.

Kwa upande wake, Rais wa Wabunifu Majengo Tanzania, Mbaraka Hussein Igangula, amewataka wadau na Watanzania kubadili mtazamo wa matumizi
ya vifaa kutoka nje na kuanza kutumia vinavyozalishwa nchini.

Amesema wapo wadau wa ujenzi ambao badala ya kutumia vifaa kutoka nchini wanapendelea zaidi kutumia vile vya nje ambavyo baadhi
vinachangia sana katika kuharibu mazingira.

Post a Comment

0 Comments