Business

header ads

BENKI YA DUNIA KUSAIDIA MIRADI MBALIMBALI TANZANIA

Serikali ya imewekeana saini ya mkopo wa shilingi bilioni 710 na Benki ya Dunia kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo katika miji mikuu ya Tanzania.
Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile amesema kuwa fedha hizo zimegawanywa sehemu tatu ambapo bilioni 537.9 imeelekezwa katika kuboresha miundo mbinu ya jiji la Dar es Salaam, Bilioni 107 ikiwa ni ujenzi wa nyumba za bei nafuu na bilioni 64.5 zitatumika katika mradi shirikishi ya uvuvi.

Aidha Likwelile ameongeza kuwa atahakikisha anazisimamia taasisi husika zilizoainishwa katika mkataba huo kuwa zinapata fedha hizo na kutekeleza mipango iliyoainishwa na hivyo kuleta mabadiliko kwa nchi.Post a Comment

0 Comments