Business

header ads

ASKARI MAGEREZA WAKAMATWA NA NOTI BANDIA NA SARE ZA JESHI LA WANANCHI

Jeshi la polisi mkoani Simiyu linawashikilia askari wawili, mmoja wa jeshi la magereza na mwingine polisi baada ya kupatikana wakiwa na noti bandia zenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni moja pamoja na sare za jeshi la wananchi wa tanzania (jwtz).

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo, kamanda wa polisi mkoani humo, Charles Mkumbo, amesema askari hao wamekamatwa jana saa 9 mchana katika mtaa wa Old Maswa kata ya Nyakabindi wilayani Bariadi.

Mkumbo amewataja watuhumiwa hao ni askari wa kikosi cha FFU mkoa wa Simiyu namba H2420 PC Seleman Juma (25) na namba B.6499 WDR Edmund Masaga (28) ambaye ni askari magereza wilayani Bariadi.

Kamanda Mkumbo amesema baada ya mwalimu huyo kupokea noti hizo ‘feki’ 10 zenye thamani ya Sh.100,000 akazitilia wasiwasi pesa hizo na alipoendelea kuzikagua zaidi akagundua hazifai kwa matumizi halali.


Post a Comment

0 Comments