Sura ya 7:
1.Kila jambo lifanyikalo duniani lina kanuni na miongozo; zaidi hata kanuni nazo zina miongozo na miongozo pia ina kanuni zake
2.Naam hata
salamu za kila siku zinalindwa na miongozo na kanuni,ndio maana Aina za
salamu hutegemea muda,uzito, mahusiano ya wanaosalimiana,umri,heshim a na mazoea 3.Ukiona unafanya jambo lolote na hujui
maana yake ama kwanini unalifanya jambo hilo basi ujue wewe ni
"toroli"; Basi hata sasa nawasalimia maana naamini mnajitambua na
mnatambua nyakati hizi 4.Nayaona maswali kadhaa kichwani mwako, ndio
nayo hayo maswali yamejengwa katika kanuni na miongozo fulani uliojengwa
nayo,hata kama umekariri bila kujijua kuwa unaziamini kanuni hizo
5.Eeeh kijana Je unajitambua? Je unajua kama maisha yako yanaongozwa na
miongozo na kanuni? Je unajua kuwepo tu kwa aitha kanuni au miongozo
mibovu juu ya jambo lolote maishani ni "ukengeufu"? 6. Unaweza
kutafakari na kutafasiri uwezavyo au ujuavyo juu ya "Elimu",ila amini
amini nakwambia kuwa "Elimu ni lugha tu" Ni lugha inayokufanya wewe
uweze kuwasiliana na "wewe", wengine na mazingira yako 7. Kwasababu ya
Elimu tunajua yapo madini ya thamani miambani,naam vidubuwasha viitwavyo
seli viiundavyo mwili na Kwamba kati ya wale wapo vichaa wenye nafasi
ya kuwaongoza walio timamu 8.Yako mambo yanishangazayo kwa vijana wa
kileo waliobahatika kupata tu japo kajiufahamu kadogo kuhusu elimu ile
isiyo na mama yake hapa nchini mwetu, Nayo ni zaidi ya vile vituko vya
watu wa siku hizi ambao hung'ang'ania kuwaongoza wananchi baada ya
kuchakachua uchaguzi hata kama wananchi wote wanagoma 9.Watu hawa
husahau kuwa hakuna uongozi bila wananchi na hakuna kikao cha amani bila
hao, ukikomaa kuwa kiongozi wa wananchi wasiokitutaka,ni nini hasa
unataka? 10.Naam elimu hii imesaidia sana kuwafanya vijana kuwadharau
wakwao,sio wa mtaani kule kijijini tu bali hata wa kanisani kule
walikolelewa kabla hawajakuwa watu kabisa 11.Elimu hii imewafanya vijana
kujiona ghali na majinuni kuliko hata KWELI yenyewe, ikumbukwe kuwa
hakuna Maarifa yoyote duniani yaliyo juu ya Kweli, Mmh vijana hawataki
tena kukaa wala kuwekeza kijijini,hawawezi kujotolea kwa jamii yao na
hata kuona aibu kupigia picha kanisa lile ya mabati la kule kijijini
12.Masikini elimu hii imewafanya vijana kujitenga na ndugu na wazazi wao
kiuhalisia ingawa katika macho ya mazoea ya kawaida huonekana kama wako
pamoja 13.Kama zamani ulikula na nduguzo watano wote kwa pamoja kwa
kufinya ugali ndani ya sinia moja,iweje leo uone ni ushamba, uchafu na
kukosa ustaarabu baada ya kujifunza kula kwenye sahani yako huko mjini
na hata hujanunua hata sahani moja kuleta nyumbani? 14. Eti umerudi
nyumbani na kompyuta mpakato hivyo sasa kazi za nyumbani hufanyi maana
uko bize na "kazi" ambazo kihalisia ni filamu na mitandao ya kijamii,na
kwakuwa hakuna ajuaye basi umeinuliwa ma kutukuzwa kwelikweli 15. Elimu
hii jamani imekufanya usiwahi kanisani tena sembuse kufanya usafi?
Huwezi kuhudhuria shughuli yeyote ya kijamii,hutaki kujitolea kuchimba
kaburi mwingine akitangulia sembuse kuhudhuria tu basi! 16.Heshima
imeshuka na maadili yanazidi kubomoka,mmh sasa vijana wanaweza kuoana
mara nyingi wawezavyo wakiwa chuo....ndio maana lile huitwa "tendo la
ndoa" na mabinti nao huyaanika maziwa yao nke,kitu gani kuvaa nguo za
kulalia hata kanisani? 17. Ikiwa hata elimu hiyo tu ilikamilishwa kwa
rushwa na uwizi wa kuiba ripoti za kale na kujifanya umefanya utafiti
karibuni, hahahahaha unawezaje kumshukuru Mungu kukusaidia kumaliza chuo
salama hali unajua wakufunzi kadhaa wanaujua utupu wako ili ufaulu? 18.
Mbona elimu imekufanya uone maisha yako mjini tu? Kwanini kutamani
kutoa Ushuhuda wa kununua gari kali bila kuwa tayari kuelezea mchakato
wa muujiza huo? 19. Elimu ya chuo ni nzuri na muhimu na madarasa yake ni
ya kitambo tu,sasa una bahati mbaya sana kama unaona elimu hiyo ni
mbingu nzima na kila aliyeikosa yuko duniani 20.Jamii yako ni mahali
ambapo panaitwa "mtarudi",usijisahau ukienda chuo kwa miaka yeyote ile
na kuona umepaa,hali ukimaaliza utarudi hukuhuku kutafuta kazi au
kufanya biashara 21.Ikiwa elimu hiyo imekufanya urahisishe wokovu na
kumuona Mungu mjomba wako; Imekufanya bize kiasi ushindwe
kutumika,kujifunza hata kuomba; Imekufanya urahisishe dhambi kwa jina la
makosa au bahati mbaya; Imekufanya usiombe na kufunga tena na zaidi
imekufanya uwe mkristo mpagani na mchambuzi basi huo ni uharibifu wako
22. Ikiwa elimu hiyo imekufanya uhame hata kanisa lako la zamani na
kuhamia eti lile la wastarabu kama wewe,basi huna tofauti na atemaye
pipi ili kupiga mluzi 23. Eeeh kijana nimesikia habari zako na
zimenisikitisha sana,ingawa una jina la kuwa msomi mkristo ama msomi
aliyeokoka lakini kwa kanuni na miongozo ya Ulimbukeni uliombatana
nao,hakuna mahali utaleta madhara chanya hata kidogo 24. Eti siku hizi
hubebi tena Biblia ibadani maana unayo simu ya kisasa ambayo ina Biblia
ndani yake,na watu wakikuona wanaweza kujua umezama katika neno wakati
wa mahubiri kumbe uko katika mitandao ya kijamii 25. Khaa! tangu lini
ukaona ni ustaarabu kuingia ibadani ukiwa unatafuta tafuna vya kutafuna?
Ama unasalimiana na marafiki wakati maombi yanaendelea kwakuwa tu
umefika sasa hivi? 26.Je unazijua vema kanuni za uhalisia na miongozo
asili ya kila aliyejitambua? Ni nani alikwambia kuwa elimu ua chuo kikuu
inamfanya aliyeipata kuwa thamani kubwa mara mia zaidi ya wale
walioikosa? Kwanini kujifanya jemedari kila mahali kwasababu ya hako
kajielimu kako? 27.Zipo kanuni kadhaa zinazoweza kuongezwa katika zile
za binafsi na hizo zinaitwa "kanuni za maisha", zimenifaa sana mimi
binafsi maishani na hata sasa zitafaa kwako kama ukinitambua 28.Naam!
Jitahidi kudaka kila taarifa muhimu kila siku maishani; Weka msisitizo
na vipaumbele kwa yale yahusuyo HATMA yako; Uwe na nidhamu binafsi kwa
yale uyapangayo na uyaamuayo; Fanya tathmini mara kwa mara ya matokeo
mbalimbali ya maamuzi yako na Uwe mwajibikaji kwa kila lile uonalo ni
haki yako 29. Awezaye kuona yasiyoonekana,anaweza kufanya yasiyowezekana
30.Katika maisha yapo mambo ambayo ni "Muhimu" na ni "Lazima" mfano
Kupata Chakula; Pia yapo mambo ambayo ni Muhimu lakini sio Lazima;
Mengine Ni Lazima ila sio muhimu na yapo ambayo Sio Muhimu na wala sio
lazima mfano kushinda ukiangalia filamu 31.Mara zote ufanyapo lolote ni
muhimu kujua hasa yale ufanyayo yanasimamiwa na kanuni zipi na miongozo
ipi ili usije kuwa mhanga wa kuamini kuwa unaweza kupika kwa mwanga wa
tochi 32.Hakuna elimu wala ujuzi ulio juu ya Neno na neno la Mungu wala
mungu mwingine juu ya Mungu KWELI na hakuna Vazi lolote linaloweza kumpa
mtu thamani zaidi ya vazi la wokovu 33. Unaweza kuvaa suti kali ya
kisomi,mtazamo na kiburi chako cha shahada kikakufanya ubaki kuwa
mwanadini mwaminifu katika kila ibaada,maana kila unapowaza
kutubu,kusifu ama kuabudu huachi kujiwazia kuwa wewe ni msomi na nguo
zako za ghali zaweza kuchafuka 34. Mpaka pale utakapoacha kumwabudu
Bwana kwa kanuni na miongozo ya kimazoea hususani yenye nakshi za
usomi,Utamuona Mungu maishani mwako katika viwango visivyo vya kawaida
35.Elimu sawia kwa kijana aliyejitambua na mwenye uwezo wa kusoma leo na
kesho ya jamii yake vema ni chachu ya harakati za kuwaletea wananchi
maendeleo na kijana akiwa na Neno ndani yake basi hakuna Awezaye
kuingusha hekima yake!
36. Niseme nini juu ya kukusisitiza kupata elimu kwa namna yeyote halali iwezekanavyo kwa juhudi zote ila tu chunga elimu hiyo isikuhamishe mstarini kamwe 37.Iliandikwa tangu kale kuwa " mshike sana elimu usimuache aende zake maana ndio uzima wako" zaidi ya hapo kumbuka "wakati"ni rasilimali isiyoweza kubadilishwa katika mfumo bali kufuatana nayo tu 38.Usijitee kwa kisingizio cha kumtumikia Mungu na wala kupunguza ama kuongeza alama za ufaulu zisikufanye ubweteke na kuona hapo ulipofika ndio basi tena! 39. Basi Mungu Roho Mtakatifu na alifafanushe jambo hili kwa kina,naam akusemeshe kuhusu ELIMU chini ya miongozo na juu ya kanuni za KIUFALME! 40.Na ikiwa elimu uliyoipata imekufanya udharau watu na kanisa na yamkini watumishi wa Mungu na zaidi ulizoee na kulichukulia poa Neno la Mungu basi angalia ulipoanguka ukatubu na ujifunze upya miongozo na kanuni za Kimungu,Amen!
36. Niseme nini juu ya kukusisitiza kupata elimu kwa namna yeyote halali iwezekanavyo kwa juhudi zote ila tu chunga elimu hiyo isikuhamishe mstarini kamwe 37.Iliandikwa tangu kale kuwa " mshike sana elimu usimuache aende zake maana ndio uzima wako" zaidi ya hapo kumbuka "wakati"ni rasilimali isiyoweza kubadilishwa katika mfumo bali kufuatana nayo tu 38.Usijitee kwa kisingizio cha kumtumikia Mungu na wala kupunguza ama kuongeza alama za ufaulu zisikufanye ubweteke na kuona hapo ulipofika ndio basi tena! 39. Basi Mungu Roho Mtakatifu na alifafanushe jambo hili kwa kina,naam akusemeshe kuhusu ELIMU chini ya miongozo na juu ya kanuni za KIUFALME! 40.Na ikiwa elimu uliyoipata imekufanya udharau watu na kanisa na yamkini watumishi wa Mungu na zaidi ulizoee na kulichukulia poa Neno la Mungu basi angalia ulipoanguka ukatubu na ujifunze upya miongozo na kanuni za Kimungu,Amen!
0 Comments