Business

header ads

BOMA LA MAKUMBUSHO KUJENGWA IRINGAMkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Manzesa amesema mkoa wake utapata jengo la makumbusho la kisasa kabisa litakalokuza sekta ya utalii pamoja na kuwawezesha wajasiriamali wadogo na kuongeza ajira kwa jamii ya Iringa na pia kukuza na kuutangaza utamaduni kwa ajili ya maendeleo ya utalii kwa kanda za juu kusini.

Mkuu huyo wa mkoa amesema Nyanda za Juu kusini licha ya kuwa na vivutio vingi vya utalii, hata hivyo bado rasilimali hiyo haijatumika ipasavyo ili kuweza kuchangia katika kukuza maisha ya jamii hii kutokana na kukosekana kwa ufahamu bora miongoni mwa wanajamii juu ya umuhimu wa wa urithi huu wa utamaduni na utalii kwa maendeleo ya sekta ya utalii na biashara.

Manzesa amesema jengo hili la kisasa la makumbusho litakuwa katika iliyokuwa ikifahamina kama Iringa Boma, ambapo sasa litatumika kwa ajili ya kuonesha mambo ya urithi wa kihistoria na kuvutia watalii duniani kote kuja kutembelea Tanzania hasa mkoa wa Iringa.

Mkuu huyo wa mkoa amesema ajira nyingi zitaongezeka kuanzia ukarabari wa jengo hilo la zamani na vilevile wasomi wa taaluma ya makumbusho na uhifadhi wataajiriwa katika kuhudumia makumbusho haya ya kisasa.
 
Mapema Meneja wa mradi wa Fahari Yetu-(Southern Highland Culture Solution (Fy-ShiCS) Jan Kuver alisema kwamba mradi huo umetenga takribani shilingi 248 miliong za Kitanzania kwa ajili ya kazi hiyo ya ukarabari na uboreshaji wa jengo hilo la makumbusho ili liweze kutumika ipasavyo kwa kazi za makumbusho ya kiutamaduni.
Mkuu wa mkoa amekiomba Chuo Kikuu cha Iringa (UoI) kutumia uwezo wake wa taaluma ya tafiti ili kutoa elimu na mafunzo bora ili kuupatia mkoa wa Iringa na taifa kwa ujumla wataalamu wa mambo ya makumbusho na uhifadhi ili pia waweze kuishirikisha jamii ya mkoa huu kujihusisha na mambo utalii wa kitamaduni ambao ni urithi wetu. Chuo kikuu cha Iringa kupitia kozi yake ya Antrhopolojia ya Utamaduni na Utalii kimetoa elimu kwa viwango tofauti katika masuala ya utalii kuanzia cheti hadi shahada ya pili ya utalii.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ikishirikiana na serikali za mitaa, Chuo Kikuu cha Iringa ndio washirika wakuu wa mradi huu wa Fy-ShiCS ambao umefadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya (European Union). Makumbusho haya yatakuwa ni ya kwanza na ya pekee kwa mkoa kujikita zaidi katika urithi wa utamaduni na uhifadhi kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya utalii.

Post a Comment

0 Comments