Business

header ads

DKT. MENGI AWATAKA WANAWAKE KUTUMIA FURSA

Taasisi ya Sekta Binafsi nchini Tanzania (TPSF) imewataka wanawake wajarisiliamali nchini kutokata tamaa kutokana na vikwazo vya hapa na pale vinavyosababishwa na watu na badala yake wajione wanaweza kufanya mambo makubwa ya kiuchumi na maendeleo.

Akiongea leo jijini Dar es salaam na viongozi wa wanawake wajasiriamali kutoka vikundi na taasisi mbalimbali nchini Tanzania Mwenyekiti wa TPSF Dkt. Reginald Mengi amesema wanawake watumie fursa zilizopo kujikwamua kiuchumi.

Dkt.Mengi amesema wanawake wengi wanashindwa kufanikiwa kutokana na kuangalia zaidi vikwazo vinavyowakwamisha kufikia malengo hivyo badala yake waangalie zaidi namna ya kuviona vikwazo ni changamoto zinazoweza kuwafanuya wafanikiwe.

Post a Comment

0 Comments