Business

header ads

WANAHARAKATI WALITAKA JESHI LA POLISI KUACHA KUTUMIA MABAVUMtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini Tanzania THRDC, umelitaka jeshi la polisi nchini kuacha kutumia nguvu na mabavu kupita kiasi, wakati inapokabiliana na matukio mbali mbali ya uvunjifu wa amani ikiwemo vurugu na maandamano wakati wa uchaguzi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao huo Bi. Martina Kabisama, amesema hayo leo, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku mbili kwa maofisa waandamizi wa jeshi la polisi, juu ya umuhimu wa kuzingatia haki za binadamu, hasa kipindi hiki nchi inapoelekea kwenye matukio makuu ya kitaifa ikiwemo uchaguzi wa serikali za mitaa, kura ya maoni pamoja na uchaguzi mkuu wa urais na ubunge hapo mwakani.

Bi. Kabisama amesema mara nyingi matukio kama hayo huwa yanaenda sambamba na uvunjifu wa amani, na ni jukumu la jeshi la polisi pamoja na asasi zinazotetea haki za binadamu, kutambua matukio yanayoashiria uvunjifu wa amani ili kukaa pamoja na kuchukua hatua za kuepusha umwagaji wa damu.

Post a Comment

0 Comments