Business

header ads

WABUNIFU 10 WAKABIDHIWA FEDHA KUJIENDELEZASerikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Finland imetoa sh. Milioni 150 za Kitanzania kwa wabunifu vijana kumi katika upande wa Tehama ili kuwawezesha kuzalisha ajira kwa vijana nchini Tanzania.


Akizungumza Jijini Dar es salaam katika hafla ya kukabidhi fedha hizo kwa niaba ya waziri wa mawasiliano Sayansi na Teknolojia katibu wa Wizara hiyo Prof. Patrick Makungu amesema fedha hizo ni motisha utakaosaidia wabunifu hao kuendeleza mawazo ili waweze kutumika kwa jamii na kuleta Maendeleo.

Prof. Makungu amesema ubunifu huo utakuwa ni chanzo cha kutengeneza ajira kwa vijana kutoka kwa vijana hao ambapo wataajiri vijana wengine zaidi ili kuweza kutoa huduma husika katika jamii hivyo kuleta maendeleo katika nyanja ya sayansi na tekinolojia.
Kwa upande wao washindi wa tuzo hizo wamesema hiyo ni fursa kuu ya kujiendeleza na kuendeleza ubunifu wao katika kuboresha huduma katika jamii na kuleta ajira kwa vijana wengi wenye uwezo wa kubuni.

Post a Comment

0 Comments