Business

header ads

TUZO ZA CNN ZA WAANDISHI BORA WA AFRICA 2014


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wageni waalikwa (hawako pichani) wakati wa hafla ya kutoa tuzo za waandishi bora Afrika 2014 zilizofanyika siku ya tarehe 18 Oktoba mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, tuzo ambazo zinatolewa na CNN Multi choice.


Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya kukabidhi tuzo hizo zilizofanyika siku ya tarehe 18 Oktoba mwaka huu wakimsikiliza hotuba ya Mhe. Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, tuzo ambazo zinatolewa na CNN Multi Choice.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza
mshindi bora wa tuzo ya mwandishi mpiga picha (Photo journalist) mwandishi huru wa The Saturday Nation la nchini Kenya Bwana Joseph Mathenge wakati wa hafla ya kutoa tuzo hizo za waandishi bora Afrika 2014 zilizofanyika siku ya tarehe 18 Oktoba mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, tuzo ambazo zinatolewa na CNN Multi Choice.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili toka kuli) akiwa katikam picha ya pamoja na mshindi bora wa tuzo za CNN wakati wa hafla ya kutoa tuzo za waandishi bora Afrika 2014 zilizofanyika siku ya tarehe 18 Oktoba mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, tuzo ambazo zinatolewa na CNN Multi choice. Wa kwanza kulia ni mshindi wa tuzo hizo za CNN mwandishi huru wa The Saturday Nation la nchini Kenya Bwana Joseph Mathenge na upande wawili kushoto ni baadhi ya watendaji toka Shirika la utangazaji la CNN na  katikati ni mtoto wa mwandishi huyo.

Mshindi bora wa tuzo ya mwandishi mpiga picha (photo journalist) mwandishi huru wa
The Saturday Nation la nchini Kenya Bwana Joseph Mathenge ( wa pili kulia) akiwa ameshikilia tuzo yake akiwa na mwanae. Wa kwanza kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, na wawili kushoto ni watendaji toka CNN.
(Picha zote na Benedict Liwenga)

Na Benedict Liwenga.

TUZO za waandishi bora wa Afrika 2014 zinazotolewa na CNN Multi Choice zimetolewa rasmi siku ya tarehe 18 Oktoba mwaka huu ambapo mwandishi huru wa The Saturday Nation la nchini Kenya Bwana Joseph Mathenge aliibuka kuwa mshindi bora wa tuzo hizo.

Akiwahutubia wageni waalikwa wakati wa tuzo hizo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia alikuwa ndiye mgeni rasmi wa tuzo hizo, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alitaja jina la mwandishi huyo kuwa ndiye alikuwa mshindi bora wa tuzo hizo baada ya majaji kuamua kuwa yeye ndiye mwandishi aliyestahili kupewa tuzo hiyo kwani aliweza kupiga picha tukio la kigaidi la Wastegate lililotokea nchini Kenya na kuvuta hisia za wengi ulimwenguni.

Joseph Mathenge aliibuka mshindi bora wa kinyang’aniyo hicho kwani kwa hali isiyo yeye akishirkiana na mwanae waliweza kwenda kusaidia kuokoa maisha ya watu waliokuwa wametekwa na magaidi ndani ya jengo hilo kubwa la kibiashara ambapo pia aliweza kupiga picha zenye kuleta hisia katika jamii bila kujali hatari iliyoko wakati akifanya kazi hiyo.

Shindano hilo la aina yake ambalo pia liliwavutia waandishi mbalimbali ndani na nje ya nchi ambapo washindi hao walijishindia tuzo zao katika nyanja mbalimbali zikiwemo za mambo ya utamaduni, vipindi na taarifa za runinga na redio, uchumi, afya na madawa, nishati na miundombinu, lugha ya Kireno, tuzo ya kuripoti michezo na nyinginezo.

Baadhi ya washindi hao walioweza kuingia fainali za tuzo hizo na kuweza kujinyakulia tuzo walikuwa ni pamoja na Obinna Emelike wa Business Day (Nigeria), Patrick Mayoyo wa Daily Nation (Kenya), Safia Berkouk wa El Watan (Algeria), Sean Christie mwandishi wa kujitegemea wa Landbouweekblad na The Mail & Guardian (Afrika Kusini).

Wengine ni John Muchangi Njiru wa The Star Newspaper ( Kenya), Olatunji Olade wa The Nation Newspaper (Nigeria), Rashid Ibrahim wa Citizen Tv (Kenya), Bento Venancio wa Msumbiji, Evelyn Watta (Kenya), Anne Mawathe wa Citizen Tv (Kenya), Brito Simango wa Msumbiji, Joy Summers na Susan Comrie wa Afrika Kusini pamoja na Bheki Makhubu.

Hafla za kukabidhi tuzo hizo pia zilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo Wafanyakazi toka CNN Multi Choice nchini Marekani, Mwenyekiti wa kampuni ya IPP Media, Dkt. Reginard Abraham Mengi, mlezi wa Dar es Salaam City Press Club na Zanzibar Press Club, Altaf Hirani Mansoor na wageni wengine walioalikwa.

Shindano hilo ni la 19 ambalo liliwashirikisha waandishi wapatao 29 kutoka nchi mbalimbali za Afrika ambapo kwa upande wa Tanzania, mwandishi wa gazeti la The Guardian, Dickson Ng’hili alikuwa mwandishi wa pekee aliyefanikiwa kuingia katika kinyang’anyiro hicho.Post a Comment

0 Comments