Business

header ads

SERIKALI KUWEKA KAMERA MAALUM KUBAINI MATUKIO YA UHALIFU Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
 Wananchi wakifurahia hotuba ya  Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Masaki Okada  wakikata utepe  kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Saidi Meck Sadiki, Meya wa Konondoni Mhe, Mbunge wa Kawe  Mhe Halima Mdee, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Mhandisi Musa Iyombe na viongozi wengine
 Sehemu ya barabara  ya Mwenge-Tegeta yenye urefu wa Km 12.9, ambayo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mbunge wa Kawe Mhe Halima Mdee  baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam. PICHA NA IKULU


Serikali ya Tanzania ipo katika mchakato wa kukamilisha uwekaji wa kamera maalumu za kubaini matukio ya yote ya uhalifu ambapo mpaka kufikia Juni mwakani, vyombo vya ulinzi na usalama vitakuwa vimefikia hatua nzuri ya kubaini matukio yote yanayofanyika katika barabara na mitaa ya jiji la Dar es Salaam.

Rais wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua kipande cha barabara ya Mwenge Tegeta, chenye urefu wa kilomita 12.9, kilichojengwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na Japan na kugharimu fedha za Tanzania shilingi bilioni 99.6.

Kwa mujibu wa rais Kikwete, ufungaji wa vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara na miundombinu ya usafirishaji, ambapo ameonya kuwa siku za wahalifu wanaopora, kuiba na kudhuru watu katika mitaa na barabara za jiji la Dar es Salaam sasa zinahesabika.Aidha, rais Kikwete amewataka Watanzania kuachana na dhana potofu kuwa serikali inaweza kumaliza tatizo la msongamano wa magari katika mitaa ya katikati ya jiji la Dar es Salaam, na kwamba inachoweza kufanya hivi sasa ni kupunguza ukubwa wa tatizo hilo.

Rais amefafanua kuwa tatizo tatizo la msongamano wa magari ni la kawaida kwa maeneo yenye shughuli nyingi katika miji mikuu mbali mbali duniani, na kwamba katika jiji la Dar es Salaam, serikali inakaribia kuanza kutumia usafiri wa majini kama sehemu ya kupunguza ukubwa wa tatizo hilo.


Post a Comment

0 Comments