Business

header ads

SERA MPYA YA KUWALINDA WAZEE YATAKIWA KUZINGATIWA

Katika kuadhimisha siku ya wazee duniani Tanzania inatajwa kushika nafasi ya 92 katika orodha ya nchi zenye idadi kubwa ya wazee ikiwa ni kati ya nchi 96 duniani kote huku takwimu za Umoja wa Mataifa zikieleza kuwa ifikapo mwaka 2050 idadi yao itakuwa sawa na ya watoto Duniani kote.


Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Helpage Bi Amleset Tewodros amesema Takwimu zinaonesha kuwa katika nchi 96 duniani idadi ya wazee ambao wanaanzia umri wa miaka 60 imeongezeka hadi kufikia asilimia 91 ya idadi ya watu duniani huku asilimia 4 tu ya wazee wakipata pensheni ya uzeeni na asilimia 73 wakiachwa huku wengi wao wakitegemea kilimo kama nyenzo ya uchumi wao.

Tewodros amesema ukuaji wa uchumi pekee hauwezi kuboresha ustawi wa wazee pasipokuwepo kwa sera maalumu inayoshughulikia wazee na kueleza kuwa idadi inaongezeka theluthi ya walio katika umri wa miaka 60 wanaishi katika nchi zenye uchumi wa kati.

Hata hivyo Tewodros ameitaka serikali kuweka sera zenye kusimamia maslahi ya wazee katika afya, kipato, ulinzi na kupewa kipaumbele Katika utoaji wa huduma kwa wazee Tanzania na kueleza kwamba ukuaji wa uchumi peke yake hautaweza kuboresha ustawi wa wazee bila sera maalum kushughulikia matokeo ya uzeeni.

Post a Comment

0 Comments