Business

header ads

OSCA PISTORIOUS AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 5Oscar Pistorius akiwasili katika mahakama ya Pretoria nchini Afrika kusini kusikiliza hukumu yake leo.

Mwanariadha huyo asiye na miguu aliyeshangaza ulimwengu katika michuano ya Olympic mwaka 2012, amehukumiwa kifungo cha miaka 5 gerezani na Jaji wa Afrika ya Kusini asubuhi hii, katika hatua inayofikisha tamati mlolomngo wa muda mrefu wa kesi hiyo iliyokuwa ikifuatiliwa kwa karibu ulimwenguni kote

Pistorius alipatikana na hatia ya kuua bila kukusudia mnamo Septemba 12, mwaka huu, kwa kumtoa roho rafiki yake wa kike mwanamitindo  Reeva Steenkamp, siku ya Valentine’s Day mwaka 2013 kwa kumpiga risasi katika bafu nyumbani kwake Pretoria.

Post a Comment

0 Comments