Business

header ads

DESEMBA 7 KILELE UHURU MARATHON


Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akiongea na Wanahabari (hawapo pichani) katika ufunguzi wa mashindano ya Mbio za Riadha za Uhuru  yanayotarajiwa kuaanza  hivi karibuni jijini Dar es Salaam, wa kwanza kulia ni mratibu wa mashindano hayo Bw. Innocent Melleck na  wa kwanza kushoto ni  Katibu Msaidizi wa Chama cha Riadha Mkoani Dar es Salaam Bi. Ombeni Zavala.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel katikati akisisitiza jambo kwa Katibu Msaidizi wa Chama cha Riadha Mkoani Dar es Salaam Bi. Ombeni Zavala wa kwanza kushoto katika ufunguzi wa mashindano ya Mbio za Riadha za Uhuru


   
Chama cha Riadha Tanzania kimetakiwa  kuwajengea wachezaji fikra chanya na maandalizi bora  ili waweze kupata mafanikio katika mashindano ya Kimataifa na Kitaifa.

Hayo yamebainishwa leo na Naibu katibu mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni  na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel alipokuwa akifungua Mbio za Riadha za Uhuru  zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni jijini  Dar es Salaam ambazo zitafikia kilele chake 7/12/2014  katika viwanja vya leaders mjini dar es salaam.

Alisema michezo ya Riadha itumike kama daraja katika jamii kwa ujumla ili iweze kujenga mahusiano mema, kudumisha amani na kuenzi Muungano wetu.

Alitoa rai kwa viongozi wa riadha Tanzania kusimamia vyema mchezo huo ikiwa ni pamoja na kutafuta vijana wenye vijana  ili kuweza kupata vijana bora ambao watashiriki karika mashindano mbalimbali ya ngazi tofauti yatakayofanyika nchini na nje ya nchi.

Wakati huohuo  amewaasa  wadau,wafadhali na taasisi mbali mbali kuwa mstari wa mbele katika kuendeleza na kuchangia michezo mbalimbali ikiwemo kusaidia mafunzo na vifaa wakati wa mashindano.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Zainab Mbilo alisema michezo ni nguzo kuu katika kupunguza magonjwa na kuweka mwili katika hali nzuri pamoja na kusisitiza kwamba michezo inaleta umoja kwani hukutanisha watu wa rika tofauti katika jamii.

Nae mratibu wa mashindano hayo Bw. Innocent Melleck aliishukuru serikali kwa kuwapa moyo,mwongozo katika maandalizi ya mbio hizo kila yanapofanyika na kuyafanya kuwa bora
“Riadha ni mchezo ambao umewahi kuiletea nchi medali nyingi kwenye michezo mbalimbali ya kimataifa, ikiwamo Michezo ya Jumuiya ya Madola, Olimpiki na ya Afrika”. Alisema Bw. Melleck

Uhuru marathon ni tukio ambalo huadhimisha Siku ya Uhuru wa Tanzania huku ikiweka mkazo katika kuimarisha Amani,Upendo na Umoja.

Mwaka huu zitajumuisha mbio ndefu za kilometa 42,mbio fupi za kilometa 21 pamoja na kilometa 3 zitakazojumuisha viongozi ili kuonyesha uzalendo zikiwa mbio za tatu kufanyika tokea kuanzishwa kwake.

Post a Comment

0 Comments