Business

header ads

CHUO KIKUU ARDHI KUTATUA TATIZO LA UDHIBITI WA MAJI TAKA,TAKA NGUMU


Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Idrissa Mshoro akiwaeleza waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusu mpango wa chuo hicho wa kuendelea na jitihada za kutatua tatizo la udhibiti wa maji taka na tanga ngumu ikiwemo ujengaji wa miundombinu ya majaribio ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji na gesi asili ya kupikia, wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma wa chuo hicho Prof. Gabriel Kassenga.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi ambaye pia ndiye mtaalam wa teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka (waste treatment facilities) Dkt. Shabaan Mgana Akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) namna Teknolojia hiyo ya kubadili taka ngumu na maji taka inavyotumika na kuwasaidia wananchi walioonesha nia ya kuitumia ikiwamo kupata mboji kwa ajili ya mazao, mimea pamoja na kupata gesi asili ya kupikia, ambapo mpaka sasa kiasi cha nyumba 100 za awali katika mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na  nyumba mia moja katika Chuo Kikuu cha Ardhi zimeshaunganishwa katika Mradi huo, wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof. Idrissa Mshoro


Miundombinu ya majaribio ya teknolojia za kibiolojia zinazobadili tanga ngumu au maji taka ambayo huzalishwa majumbani kuwa mboji zilizojengwa katika maeneo ya Chuo Kikuu cha Ardhi, mtaa wa Migombani, kata ya Segerea na katika kiwanda cha Madawa ya Binadamu cha  Mansoor Daya ChemicalsMwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Ardhi Bi. Minza Selele akiwasha karatasi kwa kutumia Gesi Asili iliyozalishwa na Mtambo huo.
Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam kimesema tatizo la taka ngumu na maji taka hapa nchini limekuwa likichangiwa kwa kiasi kikubwa magonjwa ya mlipuko kama vile kuhara damu na kipindupindu na kupelekea vifo kwa wananchi kutokana na kutokuwa na mfumo bora na rahisi wa kuweza kuwafikia wananchi katika maeneo yao.

Makamu Mkuu wa Chuo cha Ardhi ,Prof.Idrisa Mshono amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akionyesha namna chuo hicho kilivyotengeneza teknolojia ya kibiolojia inayotandazwa ardhini kwa lengo la kudhibiti maji taka na taka ngumu.

Kwa upande wake Mtafiti Mwandamizi kutoka chuo kikuu cha Ardhi Dkt. Shaban Mgana amesema kupitia teknolojia hiyo ya kibiolojia taka ngumu au maji taka yanayozalishwa majumbani yatakuwa yakitumika kama mboji na gesi asilia ya kupikia majumbani


Post a Comment

0 Comments