Business

header ads

CHANJO YA MATENDE MABUSHA KUTOLEWA


Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inatarajia kufanya kampeni shirikishi ya ugonjwa wa Surua na Rubella kuanzia tarehe 18 hadi 24 oktoba, 2014.Akizungumzia kampeni hiyo jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Dkt. Donald Mmbando amesema kampeni hiyo itaambatana na utoaji wa matone ya Vitamini A, dawa za kutibu na kukinga magonjwa ya Minyoo, Usubi,Matende na Mabusha inatarajiwa kufanyika nchi nzima ambapo itawahusisha watoto wenye umri wa kuanzia miezi 9 hadi miaka 15.Dkt. Mmbando amesema kuwa lengo na madhumuni ya kampeni hiyo ni kudhibiti milipuko ya magonjwa ya Surua na Rubella ili kupunguza vifo na madhara yanayosababishwa na magonjwa hayo.

Na kufafanua kuwa chanjo hiyo itatoa fursa ya kutoa kinga kwa watoto wengi zaidi ambao hawakupata chanjo hiyo utotoni katika mikoa yenye maambukizi makubwa ya magonjwa hayo.Kwa upande wake Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Dafrosa Lyimo ametoa wito kwa wazazi kuhakikisha kuwa wanawapeleka watoto wao katika vituo vya afya ili waweze kupata chanjo hiyo.Pia ametoa wito kwa mama wajawazito kuhakikisha kuwa wanapata chanjo ya Surua-Rubella ili kuwakinga watoto wao dhidi ya matatizo ya Moyo, mimba kuharibika, kujifungua kabla ya wakati na mtindio wa ubongo yanayotokana na ugonjwa huo.

Post a Comment

0 Comments