Business

header ads

ZAIDI YA WATU 35 WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA MABASI ILIYOTOKEA MCHANA HUU MJINI MUSOMA
Watu 36 wamefariki dunia papo hapo na wengine 79 wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani baada ya basi la Mwanza Coach na JK Express kugongana uso kwa uso pamoja na gari dogo katika daraja eneo la 77 wilaya ya Butiama Mkoani Mara.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamishna wa Polisi  wa mkoa Mara Philip Kalangi amesema ajali hiyo imehusisha basi lenye nambari za usajili T677 CYC mali ya kampuni ya J4 express lililogongana uso kwa uso na basi limhine la kampuni ya Mwanza Coach lenye nambari za usajili T736 AWJ katika eneo la SabaSaba mjini Musoma. 
 
Kamanda Kalangi amesema Watu zaidi ya 36 wamepoteza maisha papo hapo na wengine zaidi ya 79 kujeruhiwa vibaya. Hata hivyo kamanda huyo amesema bado wanaendelea kufanya uchunguzi wa ajli hiyo ili kutoa ripoti kamili.


Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali Grace Massawe hiyo ameeleza chanzo cha ajali hiyo ni basi la J4 ambalo lilikuwa likijaribu kuipita gari ndogo aina ya Nissan lenye nambari za usajili T 332 AKK katika sehemu ambayo mbele kuna daraja linaloweza kupitisha gari moja kwa wakati huo,kutokana na kuwa basi hilo lilikuwa kwenye mwendo kasi,liliisukuma ubavuni gari hiyo ndogo ambayo haikuweza kuhimili nguvu ya Basi hilo na kutoka kwenye njia na kwenda kuingia mtoni.
Basi la Kampuni ya MWANZA COACH lililokuwa likitokea Musoma kwenda Mwanza linavyoonekana baada ya kugongana uso kwa uso na Basi la Kampuni ya J4 EXPRESS.
Umati wa Watu ukiwa umekusanyika kwenye eneo hilo ilikotokea ajali hiyo mbaya na kusababisha watu 35 kupoteza maisha hapo hapo,wakishuhudia tukio hilo la ajali.


Buldoza likifanya kazi ya kuichomoa gari ndogo aina ya Nissan Terano lenye nambari za usajili T 332 AKK lililoshukumwa na basi hilo mpaka kuingia mtoni.Gari hii ilikuwa na watu watatu,ambapo wawili wamefariki dunia na mmoja kujeruhiwa.

Sehemu ya waokoaji waliofika kwenye tukio hilo.
Wanausalama wakijadiliana jambo kwenye eneo hilo la tukio.

Baadhi ya Mizigo ya abiria wa mabasi hayo wakiwepo waliopoteza maisha.
Uokoaji ukiendelea.
Askari Polisi wakitoa miili ya watu wawili waliokuwemo kwenye gari hiyo.

Post a Comment

0 Comments