Business

header ads

WANANCHI WATAHADHARISHWA VISHOKA WA UPIMAJI ARDHI


Mkurugenzi Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mikazi Bw. Justo Lyamuya akizungumza na 
waandishi wa habari kuhusu taratibu za upimaji wa viwanja nchini Kushoto ni Katibu wa Baraza la Upimaji na Uthamini wa Wizara Hiyo Bw. Nassor 
DudumaKatibu wa Baraza la Upimaji na Uthamini wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mikazi Bw. Nassor Duduma akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu ufuataji wa Sheria katika shughuli za upimaji ardhi kwa mujibu wa Sheria ya mwaka 1957 sura namba 324, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Afisa Habari wa Wizara Hiyo Bw. Clarence Nanyaro.
Serikali imewataka wananchi kujihadhari na makampuni yanayojiingiza katika kazi za upimaji ardhi na tathimini bila ya kusajiliwa  na bodi au Halmashauri zenye mamlaka ya kusimamia taaluma husika.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi bw. Justo Lyamuya wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliolenga kutoa utaratibu unaotakiwa kufuatwa na wananchi katika upimaji ardhi.

Hadi sasa wapima ardhi waliosajiliwa ni 290 wakati makampuni yaliyosajiliwa na Baraza la Taifa la wapima na wathamini ardhi ni 58” hivyo hakuna haja ya wananchi kutapeliwa na vishoka. Alisema Bw. Lyamuya.
Lyamuya amesema kuwa ni vyema wananchi wakatumia makampuni yaliyosajiliwa kufanya kazi ya kupima ardhi ili kuepuka migogoro ambayo kwa kiasi kikubwa inachangiwa na ukiukwakwaji wa sheria na taratibu za upimaji ardhi.
Aidha Lyamuya akitoa ufafanuzi kuhusu wathamini (valuers) amesema hadi sasa wataalamu waliosajiliwa ni 320 na makampuni yalisajiliwa na Baraza ni 54.
Pia Lyamuya alisema kuwa kazi za upimaji viwanja zitakazowasilishwa Wizarani ambazo hazikufuata taratibu na kwa mujibu wa sheria ya upimaji Ardhi sura 324 ya mwaka 1957 hazitapokelewa. Ambapo ameeeleza mambo yanayopaswa kuzingatiwa katika upimaji wa ardhi (mashamba na viwanja) lyamuya amesema upimaji usiozingatia ushirikishwaji na kutambua mipaka kwa maridhiano hautapokelewa.

Hata hivyo, makampuni ya upimaji yanayowasilisha kazi za upimaji kwa Mkurugenzi waUpimaji na Ramani ambazo hawakuzisimamia wao wenyewe au wawakilishi wao na kudhibitika, kazi hizo hazitapokelewa na kwa mujibu wa sheria za kusajili makampuni ya upimaji Na.2 ya mwaka 1977 yataadhibiwa ikiwa ni pamoja na kusimamishwa.Post a Comment

0 Comments