Business

header ads

VIJANA WAASAWA KUACHA KUENDEKEZA NGOMA ZA USIKU


Tabia ya baadhi ya vijana kupenda kwenda kwenye ngoma za usiku na zisizo na maadili maarufu kama kigodoro na kangamoko, imetajwa kuchangia ongezeko la maambuki ya virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi miongoni mwa vijana wengi nchini Tanzania.Afisa Uragibishi kutoka baraza la taifa la watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi NACOPHA Bi. Lilliane Chovenye, amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo yaliyofadhiliwa na shirika la kimataifa la idadi ya watu UNFPA, mafunzo yanayotolewa kwa vijana waathirika wa UKIMWI, kuhusu afya ya uzazi, na namna vijana hao wanavyoweza kuwa wawazi kuhusu afya zao, pale wanapokwenda kupata tiba katika vituo vya kutolea tiba.

Kwa upande wake, mmoja wa waathirika hao msichana Rosemary Sabius amesema vijana wengi nchini wamejikuta wakipata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutokana na kutozingatia mafunzo wanayopata kutoka kwa wazazi, walezi pamoja na watu waliowazidi umri, hasa mafundisho yanayowataka kutojihusisha na ngono zembe.

Post a Comment

0 Comments