Business

header ads

VIJANA MIAKA 15-24 WAONGOZA KWA UKIMWIMratibu  wa  Programu maalum za Tume ya Kudhubiti  Maambukizi  ya  UKIMWI Tanzania  (TACAIDS)  Bw.Renatus  Kihongo (katikati  akiongea   na  Wanahabari kuhusu  uwekaji  wa vituo  vya  kutoa  elimu  ya kujikinga  na  maambukizi  ya  virusi  vya  Ukimwi    katika  vituo  vya  madereva  wa  magari  yanayosafiri  safari  ndefu.wa  kwanza  kutoka   kushoto   ni  Afisa  Habari wa  TACAIDS   Bwana  Godlease Malisa   na  wa  kwanza  kutoka   kushoto  ni  Bi. Nadhifa  Omar
Kundi la vijana wenye umri wa kuanzia miaka 15 hadi 24 nchini Tanzania limetajwa kuongoza kwa kuwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi hali inayochangiwa na vijana wenyewe kutotumia kondom wakati wa kujamiiana.


Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na mratibu wa mipango maalum kutoka tume ya kudhibiti ukimwi nchini Tanzania TACAIDS Bw. Renatusi Kihongo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya ukimwi nchini.

Bw. Kihongo ameyataja makundi makubwa ya vijana ambayo yamepata maambukizi ya ukimwi kuwa ni pamoja na kundi la vijana wanaojidunga, vijana wanaofanya ngono kinyume na maumbile pamoja na kundi la watu wanaofanya biashara ya ngono ambapo mkoa wa Njombe unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu walioathirika na virusi vya ukimwi kwa nchi nzima.

Post a Comment

0 Comments