Business

header ads

TEA YATUMIA BIL 11 KUNUNUA VITABU

Mamlaka ya Elimu nchini Tanzania TEA imetumia zaidi ya shilingi bilioni 11 katika kipindi cha miaka 10 kwa ajili ya kutoa ufadhili wa kununulia vitabu vya kiada kwa shule za sekondari hapa nchini.


Afisa uhusiano wa TEA Silvia Lupembe amesema hayo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizungumza na East Africa Radio juu namna mamlaka hiyo inavyosaidia katika kukabiliana na tatizo la uhaba wa vitabu kwa shule za sekondari nchini.

Amesema TEA inatambua changamoto zilizopo kwa sasa katika sekta ya elimu hasa ya upungufu wa madawati, upungufu wa vitabu vya kiada pamoja na upungufu wa vyumba vya maabara hivyo mamlaka hiyo itahakikisha inasaidia kupunguza matatizo hayo kwa lengo la wanafunzi waweze kupata elimu iliyo bora.

Post a Comment

0 Comments