Business

header ads

SIKU YA AFYA YA MOYO DUNIANI: TAHADHARI YATOLEWAWatanzania wametakiwa kuchukua tahadhari kwa kutojihusisha na matendo hatarishi ambayo huchochea kukuza hatari za kupata ugonjwa wa Moyo ambapomagonjwa hayo husababisha vifo kwa takribani watu milioni 17. 3 duniani kila mwaka.


Akiongea leo jijini Dar es salaam, Daktari bingwa wa magonjwa ya Moyo wa Hospitali ya taifa ya Muhimbili Dkt. Delilah Kimambo amesema ili kupunguza athari za kupata ugonjwa wa moyo, watu kula chakula bora,kufanya mazoezi na kuacha kuvuta sigara,.

Dk Kimambo amesema siku ya afya ya moyo duniani ilianza ikiadhimishwa kutokana na magonjwa ya moyo kusambaa na kuongoza kwa vifo duniani na kuongeza kuwa ikiwa elimu ya uelewa kuhusu ugonjwa wa moyo itatolewa ipasavyo utapunguza idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huo. 

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha Tiba ya moyo cha Muhimbili Dk. Robert Mvungi amesema kwa sasa Hospitali hiyo inatoa huduma kwa wagonjwa wenye matatizo ya moyo na kueleza kuwa ni vyema Watanzania wakajijengea tabia ya kupima afya zao ili waweze kuanza tiba mapema. 

Post a Comment

0 Comments