Business

header ads

SERIKALI YA TANZANZANIA YAFUNGULIWA KESI YA UKIUKWAJI WA HAKI ZA BINADAMU

Kamati ya Msaada wa Kisheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam imefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa madai ya kuhusika katika ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu.

Kesi hiyo iliyofunguliwa kwa kushirikiana na Shule Kuu ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, inahusu ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na serikali kupitia kwa aliyekuwa waziri wa afya Dkt Aron Chiduo, ambaye aliruhusu kufanyika kwa majaribio ya chanjo ya ugonjwa wa Ukimwi kinyume na taratibu.


Msingi wa kesi hiyo unatokana na madhara waliyoyapata watu waliotumika katika majaribio ya chanjo hiyo ijulikanayo kama Virodene P058 iliyotengenezwa na kuletwa nchini na kampuni ya Virodene Pharmaceutical PTY ya nchini Afrika Kusini.

Chanjo hiyo inadaiwa kuleta madhara mbali mbali ya kiafya kwa waliofanyiwa majaribio hayo ambapo kati ya watu zaidi ya sitini waliofanyiwa majaribio, wengi wamepoteza maisha na hivi sasa wamebaki watu saba tu ambao nao wanalalamika kupatwa na madhara mbali mbali.

Waathirika wa chanjo hiyo ambao kimsingi ndio walalamikaji wakuu ni Bw. Steven William Kimaro, Bahari Sefu, Juto Ramadhani, Ahmed Said Mwiru, Dickson Masena, Octavunus Francis Dupya na Mhando Haji Majuwe.

Post a Comment

0 Comments