Business

header ads

MKUTANO WA BARAZALA LA MAWAZIRI EAC KUFANYIKA ARUSHAMkurugenzi Msaidizi Idara ya Biashara kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Abdulla Makame Akiwaeleza waandishi wa Habari(hawapo pichani) Kuhusu Mkutano wa 29 wa Baraza la Mawaziri wa nchi  wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika Septemba 20 mwaka huu Jijini Arusha.
Mkutano wa 29 wa Baraza la Mawaziri wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unatarajiwa kufanyika nchini Tanzania ukiwa na lengo la kuidhinisha aina mpya ya hati ya kusafiria za kielekroniki zikiwemo za kibalozi, za maofisa na za kawaida.

Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Biashara,Uwekezaji na shughuli za uzalishaji wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Makame  ambapo amesema kuwa mkutano huo utakaofanyika Septemba 20 mwaka huu Jijini Arusha

Dkt. Makame amesema mkutano huo unatarajia kupokea na kuidhinisha taarifa mbalimbali sambamba na kutolea maamuzi masuala yanayohusu mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aidha, Makame amesema mambo mengine yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na mapendekezo na hadidu za rejea za uanzishwaji wa Dira ya maendeleo ya Afrika Mashariki ya mwaka 2050 na mapendekezo ya mpango mwelekeo na shughuli mbalimbali zinazolenga kuandaa katiba ya shirikisho la Afrika Mashariki na kujadili mapendekezo ya baraza la ulinzi na usalama linalopendekezwa.

Baraza la Mawaziri katika Jumuiya ya Afrika mashariki ni chombo cha pili katika ngazi za kufanya maamuzi ndani ya Jumuiya ya  Afrika Mashariki baada ya Mkutano wa Kilele.

Post a Comment

0 Comments