Business

header ads

JESHI LA POLISI TANZANIA LATAKIWA KUANGALIA UPYA UTENDAJI WAKEJeshi la polisi nchini Tanzania limetakiwa kujiangalia upya katika utendaji wa kazi zake na kuacha kukiuka haki za binadamau ikiwemo kutowapiga ama kuwatisha waandishi wa habari wakati wanatekeleza majukumu yao ya kikazi.


Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba wakati alipokuwa akitoa msimamo wa chama hicho juu ya kupigwa hadi kujeruhiwa kwa waandishi wa habari tarehe 17 mwezi huu wakati walipokuwa wakitekeleza majukumu yao nje ya Jengo la Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.

Aidha Prof Lipumba amelalamikia kitendo cha jeshi la polisi kuzuia mikutano ya vyama vya upinzani ukiwemo mkutano wa CUF wa Bububu Zanzibar kwa madai kwamba bunge la katiba linaendelea.

Post a Comment

0 Comments