Business

header ads

DKT BILAL MGENI RASMI MKUTANO WA TAASISI ZA KODI AFRIKA

Dkt. Bilal kuwa mgeni rasmi mkutano Mkuu wa Taasisi za Kodi Afrika.

Muwakilishi wa Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) Bi. Fazila Malaherbe akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) faida za Mkutano Mkuu wa Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) ikiwemo kubadilishana uzoefu na kuwajengea uwezo wakusanya kodi wa ndani, wakati wa Mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade.


Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Rished Bade akiwaeleza waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano Mkuu wa Taasisi za Kodi Afrika (ATAF), wakati wa Mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Muwakilishi wa Taasisi za Kodi Afrika (ATAF) Bi. Fazila Malaherbe.


Makamu wa Rais Mh. Dk. Mohamed Gharib Bilal anatarajiwa kuwa mgeni rasmi  wakati wa mkutano Mkuu wa Taasisi za Kodi Afrika (Africa Tax Admistration forum-ATAF) utakaowahusisha wataalamu wa masuala ya Kodi kutoka Sehemu mbalimbali Duniani.

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es salaam na Kamishana Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) bw. Rished Bade  wakati wa mkutano na waandishi wa habari. ambapo amesema Mkutano huo unatarajiwa kufanyika kuanzia septemba 16 mwaka huu  jijini Dar es salaam.
“Lengo la mkutano huu ni kujadili namna ya kuimarisha taasisi za Kodi Africa na kuwajengea uwezo watumishi katika taasisi za kodi” alisema Bade
Akifafanua  Bade amesema ATAF  ni chombo cha Kimataifa kinachotambuliwa na jumuiya za Kimataifa kinachojihusisha na masuala ya kodi ambapo Tanzania itanufaika na mkutano huo kwa kupata fursa ya kujitangaza Kimataifa.
Katika kuzijengea uwezo nchi za Afrika Bade  amesema ATAF inalenga kuboresha Mamlaka  za Mapato lengo likiwa ni kukuza mapato ya ndani yatokanayo na kodi .
Akitaja  baadhi ya mada zitakazowasilishwa Bade alisema kuwa ni pamoja na Uongozi katika Agenda ya Kodi Kimataifa na taswira ya Taasisi za Kodi Afrika.
Pia  Bade alisema kuwa wataalamu wa Kodi watabadilishana uzoefu wa kukusanya kodi katika sekta mbalimbali pamoja na kubadilishana taarifa muhimu za biashara za kimataifa na uwekezaji katika nchi za Afrika.
Tanzania imekuwa mwanachama wa ATAF  tangu mwaka 2009 ambapo nchi wanachama ni Benin,Botswana,Burkina Faso,Burundi, Cameroon,Chad,Comoros,Egypt,Eritrea,Gabon,Gambia,Ghana.
Nchi  nyingine ni Ivorycoast,Kenya,Lesotho,Liberia,Madagasca,Malawi,Mauritania,Mauritius,Morocco,Mozambique,Namibia,Nigeria,Rwanda,Senegal, Seychelles,Sierra leone,South Afrika,Sudan,Uganda,Zambia na Zimbabwe na  Tanzania.


Post a Comment

0 Comments