Business

header ads

DK. MENGI AWATAKA WANAWAKE KUWA NA MACHO YANAYOONA FURSAMwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini Tanzania TPSF, Dk. Reginald Mengi jana amewataka wanawake nchini Tanzania kujitambua na kuondokana na dhana ya kuwa kazi za uchimbaji madini ni kazi za wanaume pekee na kuondokana na fikra hiyo kutawafanya wanawake kujijengea uwezo wa kujitegemea kwa kujihusisha na uendelezaji wa rasilimali zilizopo


Dakta Mengi ametoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam na wakati akifunga mkutano mkuu wa siku mbili wa chama cha wanawake wachimbaji madini Tanzania (CHAWOMA), na kuainisha kuwa wanawake wanaojishughulisha na uchimbaji madini ni mashujaa kwani wamefahamu fursa itakayowaondolea umaskini.

Dk Mengi amesema wanawake wanatakiwa kutambua kuwa nchi ya Tanzania sio maskini na kuwataka kuwa na macho yanayoona fursa na utajiri uliopo nchini na kuitaka serikali kuwasemehe tozo wachimbaji wadogo wadogo kwani tozo wazotozwa haziendani na dhima ya serikali ya kuzalisha ajira nchini

Post a Comment

0 Comments