Business

header ads

RAIS KIKWETE KUFUNGUA KIKAO CHA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI


Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania kesho kutwa Jumatano anatarajiwa kufungua mkutano wa kwanza na kikao cha tatu cha Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kitakachofanyika jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Karimjee.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Dkt. Margaret Nantongo Zziwa amesema mara baada ya kufunguliwa kwa mkutano huo wabunge watajadili miswada kadhaa ambayo ipo mbele ya kamati za bunge hilo ikiwa pamoja na muswada wa elimu.

Kwa upande wao Mbunge wa bunge hilo kutoka nchini Rwanda Mh. Patricia Hajabakiga na Mbunge wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki Mh. Adam Kimbisa wamezungumzia umuhimu wa kikao hicho kufanyika jijini Dar es Salaam na si katika jiji la Arusha ambapo ndiko Makao Makuu ya Jumuiya hiyo

Post a Comment

0 Comments