Business

header ads

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MAJAJI WAPYA 20 WA MAHAKAMA KUU YA TANZANIA Rais Jakaya Mrisho Kikwete,  Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali, Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda,  Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha-Rose Migiro, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu,  Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi
Ombeni Sefue, Mwanasheria Mkuu Jaji  Frederick Werema, Mtendaji Mkuu wa Mahakama Mhe Hussein kattanga  katika picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama kuu ya Tanzania baada ya kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete  akiwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu pamoja na  Majaji wa Mahakama ya Rufaa Tanzania na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wapya

  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi   Shaban Ally Lila wakiwa na Majaji wapya 
 Rais Kikwete na Waziri wa Sheria na Katiba Dkt Asha Rose Migiro wakiwa wa wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wanawake wapya
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu na Jaji Kiongozi   Shaban Ally Lila wakiwa katika pic ha ya jumla na Majaji wapya na wa zamani. 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania leo amewaapisha majaji wapya 20 wa mahakama kuu ya Tanzania akiwemo aliyekuwa mkurugenzi wa mashtaka ya Umma nchini (DPP) Eliezer Feleshi.

Majaji hao wameteuliwa na Rais Jakaya Kikwete Agosti 13 mwaka huu na uteuzi wao umejumuisha watumishi wa mahakama na mawakili wa serikali wa kujitegemea pamoja na watumishi wa taasisi mbali mbali za serikali.

Hafla hiyo iliyofanyika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam imehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali akiwemo Makamu wa rais Dk. Mohamedi Gharib Bilal, waziri mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda, pamoja na Jaji mkuu wa Tanzania Othmani Chande.


Post a Comment

0 Comments