Business

header ads

LHRC YATOA TAARIFA KUHUSU MWENENDO WA MCHAKATO WA UTUNGAJI WA KATIBA MPYA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-Bisimba, akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mwenendo wa mchakato wa utungaji wa Katiba Mpya ya Tanzania unaoendelea Dodoma.
Mtetezi wa Haki za Wanawake Ananilea Nkya, akizungumza katika mkutano huo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-Bisimba (kulia), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu mwenendo wa mchakato wa utungaji wa Katiba Mpya ya Tanzania unaoendelea Dodoma. Kushoto ni Mtetezi wa Haki za Wanawake, Ananilea Nkya.
Mtetezi wa Haki za Wanawake, Ananilea Nkya (katikati), akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Ofisa Mipango kutoka Taasisi ya Sikika, Patrick Kinemo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-Bisimba
Mwanasheria wa LHRC, Harold Sungusia (katikati), akitoa ufafanuzi wa kisheria kuhusu mchakato huo wa Katiba Mpya. Kulia ni Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Uwajibikaji wa LHRC, Imelda Urrio na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk.Helen Kijo-Bisimba.

Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Mwanasheria wa LHRC, Harold Sungusia (kulia), akionesha Katiba ya nchi wakati akizungumza na wanahabari.Katika taarifa hiyo iliyosomwa na mkurugenzi wa kituo hicho Bi. Hellen Kijo-Bisimba amesema LHRC kushirikiana na wadau wamefuatilia kwa karibu mchakato wa katiba mpya katika bunge la katiba lililoanza Agosti 5 mwaka huu bila ya baadhi ya wajumbe hasa wale wa kutoka UKAWA ambao walijitoa kwa madai ya kutoafiki mwenendo wa vikao vya Bunge la katiba.


Bisimba, amesema wanasikitioshwa na kauli za baadhi ya viongozi wa serikali pamoja na baadhi ya wajumbe wa bunge maalum kuhusiana na machakato wa katiba nchini Tanzania. Ambapo kauli hizo na matamko hayo yanaashiria mwelekeo mbaya kwa kuwa unakiuka misingi ya demokrasia na utawala wa sheria, kuminya uhuru wa vyombo vya habari na haki ya kutoa maoni na pia kwa kiwango kikubwa yanakiuka haki za binadamu


Kwa mujibu wa Bisimba ameyataja baadhi ya matamko hayo yakiwemo agizo la kupigwa marufuku mijadala ya katiba nje ya bunge la katiba, Zuio kwa vyombo vya habari kutangaza mijadala ya katiba, Majaribio ya kuzuia waliokuwa wajumbe wa  Tume ya katia kuelimisha wananchi juu ya maudhui ya Rasimu ya pili ya katiba na Mabadiliko holela ya kanuni za Bunge la katiba.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amelitaka Bunge la katiba pamoja na serikali kuheshimu uhuru wa kutoa maoni na kupokea habari. Na kuepuka kutoa kauli ambazo zitakuwa chanzo cha kuzorotesha umoja na amani kwa Taifa la Tanzania.
Imeandikwa na Materu mmiliki wa mtandao huu na mwandishi wa habari 0758131487

Post a Comment

0 Comments