Business

header ads

KUKWAMA KWA KATIBA MPYA NI DHAMBI YA KIHISTORIA

 
 Mwenyekiti wa bunge Maalumu la katiba Mh. Samwel Sitta
Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania (TSNP) umesema wanaokwamisha uundwaji wa Katiba mpya wanarudisha maendeleo ya nchi na kwamba mchakato huo haupo kwa ajili ya kuonesha misimamo ya kisiasa bali namna gani taifa litaongozwa na Katiba iliyotokana na mawazo yao.


Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Mtandao huo, Bw. Alphonce Lusako ambapo ameeleza kuwa endapo mchakato wa kupata katiba mpya utakwama itakuwa ni dhambi ya kihistoria ambayo haitaweza kufutika machoni pa watanzania.

Aidha, Lusako ameongeza kuwa kutofautiana ni demokrasia lakini demokrasia safi ni ile inayojenga muafaka, maridhiano na makubalianao na sio kubomoa na kuwataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba watambue sheria kuu ndani ya bunge hilo ni kuboresha Katiba ya wananchi.

Post a Comment

0 Comments