Business

header ads

JUKUMU LA WATANZANIA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIANCHIWaziri wa  Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt  Binilith akizunguza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam kuhusu mkutano  wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya nje kutoka nchi za kamati ya wakuu wa Nchi za Afrika unatarajiwa kufanyika Agosti 29, 2014 nchini.


Mkurugenzi  Msaidizi wa   Idara ya Mazingira Richard Muyungi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari  kuhusu mabadiliko ya tabianchi leo jijini Dar es Salaam ambapo Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano  wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya nje kutoka nchi za kamati ya wakuu wa Nchi za Afrika unatarajiwa kufanyika Agosti 29, 2014 nchini.


Serikali ya Tanzania  imetoa wito kwa wananchi kuunga mkono juhudi za zinazofanywa katika  kupambana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi ili kupata maendeleo endelevu.
Hayo yamesemwa  jijini Dar es Salaam na Waziri wa nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt.  Binilith Mahengealipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa Mawaziri wa Mazingira na Mambo ya nje kutoka nchi za kamati ya wakuu wa Nchi za Afrika unatarajiwa kufanyika Agosti 29, 2014.
Mkutano huu wenye lengo la kujadili na kupendekeza masuala muhimu  ya bara la Afrika  kuhusu upatikanaji wa fedha na teknolojia katika kukachangamoto hizo zinazo athiri sekta ya kilimo, usafirishaji, afya, nishati,mifugo,uvuvi,viwanda na maji.
“ni jukumu letu sote kuhakikisha tunakabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kwa kutumia gesi na majiko maalum ili kupunguza gesijoto inayopelekea mabadiliko ya tabia ya nchi” alisema Dkt. Mahenge
Aidha Mahenge ameongeza kuwa  nchi za Afrika zina wajibu wa kutaka nchi zilizoendelea kiviwanda ikiwemo Marekani na mataifa ya Ulaya, ziwajibike kutokana nchi hizo kutoa zaidi ya asilimia 97 ya gesi ukaa ambayo ni hatari kwa mazingira, wakati bara la Afrika likitoa asilimia 3 tu lakini ndio linaloathirika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi.


mkutano huo  ni maandalizi ya mkutano unaotarajiwa kufanyika Septemba  23, 2014 ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na ule wa 20 wa Nchi wananchama wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi utakaofanyika Mjini Lima, nchini Peru  Desemba 1-12,2014.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa   Idara ya Mazingira Suzi Salula amesema  kuwa juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi zinahitajika kutiliwa mkazo ili kuweza kujikwamua kuondokana na changamoto hii.
Ripoti ya Wataalamu wa Kimataifa  kuhusu mabadiliko ya tabianchi inaonyesha  kuwa mwaka 2013 joto la dunia limeongezeka kwa nyuzi joto 0.85 juu ya wastani wa joto la dunia na kupelekea ongezeko la gesijoto   na kuathiri  kwa kiasi kikubwa sekta ya Kilimo, nishati, afya, usafirishaji, mifugo, uvuvi, viwanda na maji.

Post a Comment

0 Comments