Business

header ads

GHARAMA WANAZOTOZA MAWAKILI ZAWA KIKWAZO Mh Jaji Shaban Lila
Serikali imetakiwa kuzitilia mkazo taasisi za huduma ya msaada wa kisheria ili kuweza kusaidia kupunguza idadi za kesi na kusaidia mahakama kurahisisha utoaji wa haki katika kesi husika.


Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Jaji kiongozi mahakama kuu ya Tanzania Jaji Shabani Ally Lila katika kongamano lililoandaliwa na Sekretarieti ya Msaada wa Kisheria (LAS) katika kujadili masuala ya kutoa msaada wa sheria katika kesi za makosa ya jinai.

Ambapo amesema kutambulika uwepo wa watoa msaada wa kisheria kutasaidia wananchi kupata suluhisho katika kesi zao mahakamani. Hata hivyo amesema kumekuwa na ongezeko la idadi ya watu nchini huku idadi hiyo ikiwa ni kubwa kuliko watoa msaada waliopo.

Aidha , Jadi Lila amesema mawakili wa kujitegemea wamekuwa ni kikwazo watu kutopata nafasi ya uwakilishi mahakamani ambapo ni mahali pa kutafuta haki, kutokana na kukosa fedha za kuwalipa ili wasimamiwe kesi zao.
Hata hivyo amezitaka taasisi zote zitoazo huduma za kisheria kuweka kipaumbele kwenye maeneo ya vijijini na maeneo mengine ambapo huduma hizo hazifiki. Na kujikita zaidi katika mashauri ya jinai haswa kwa walio katika vizuizi maana wanaouhutaji katika sheria.

Post a Comment

0 Comments