Business

header ads

CHADEMA KUCHUKUA HATUA KWA WABUNGE WASALITIChama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitawachukulia hatua kali wabunge wake iliyowaita kuwa ni wasaliti kwa kupuuza maagizo ya chama na kwenda kuhudhuria vikao vya Bunge Maalumu la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma.


Mkuu wa Kurugenzi ya Sheria ya Chadema na Msemaji wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni Mhe. Tundu Lissu amesema hayo leo jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya chama hicho kutoa taarifa ya kuwepo njama za kutaka kukidhoofisha chama hicho.

Kwa mujibu waMhe. Lissu, mamlaka ya nidhamu kwa wanachama wenye hadhi ya ubunge ni kamati kuu, chombo ambacho amesema ndiyo kilichotoa maagizo ya kwamba wajumbe wote wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA kutoka Chadema wasihudhurie vikao vya bunge maalumu la Katiba.

Post a Comment

0 Comments