Business

header ads

ASILIMIA 14 YA VIJANA WADOGO WANATUMIA DAWA ZA KULEVYAVijana wenye umri kati ya miaka 14-16 wa jijini Dar es Salaam nchini Tanzania wanaanza kutumia madawa mbalimbali ya kulevya hali inayotokana na vijana wengi kuwa katika umri wa kutaka kujua.


Akiongea Leo jijini Dar es Salaam mmoja wa vijana wanafanya uhamasishaji kwa vijana kuacha matumizi ya dawa hizo Karen Dorah amesema kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS, asiliamia 14 ya vijana Jijini Dar es Salaam wanatumia dawa za kulevya huku wengi wao wakitumia zaidi dawa za kunusa.

Kutokana na hali hiyo,Vijana hao wameitaka serikali Kufanya juhudi mbalimbali za kuwanusuru vijana kuingia katika matumizi ya dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na kuweka elimu ya dawa za kulevya katika mitaala ya shule za msingi pamoja na kuweka sheria kali kwa watu wanaobainika kusafirisha dawa za kulevya nchini.

Post a Comment

0 Comments