Business

header ads

Profesa PLO Lumumba amewataka UKAWA kurejea katika bunge la katibaMwanaharakati wa Kimataifa, raia wa Kenya Profesa PLO Lumumba amewaomba
wajumbe wa bunge maalumu la katiba kutoka kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi UKAWA kurejea bungeni na kuendelea na mchakato wa katiba mpya.


Profesa Lumumba ambaye pia ni mkuu wa bodi ya wakurugenzi wa shule kuu ya Sheria nchini Kenya, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam akiwa kama mjumbe wa jopo maalumu lililoundwa na Jukwaa la Katiba kwa ajili ya kusuluhisha na kunusuru mchakato wa katiba mpya.Katika maelezo yake Profesa Lumumba amesema idadi kubwa ya watu, wanasiasa na wadau wa katiba waliohojiwa na jopo hilo wamependekeza UKAWA warejee bungeni sambamba na kulitaka bunge hilo lijadili na kuheshimu rasimu ya katiba iliyo mbele yao pamoja na baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kuacha lugha ya matuzi, kebehi na fedheha.


Post a Comment

0 Comments